Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa inapenda kuutaarifu umma wa watanzania
kuwa, kutakuwa na kikao cha kawaida cha Baraza la Vyama vya Siasa,
kitakachofanyika Januari 18, 2018 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi.
Kikao hichokitafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkwawa, uliopo
katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo Barabara ya Shaabani Robert mkabara
na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa , Jijini Dar –es salaam.
Pamoja
na ajenda zingine zilizoandaliwa, wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa
watapata fursa ya kujadili mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria mpya ya
Vyama vya Siasa, kujadili mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni za
usajili wa Vyama vya Siasa na pia watafanya uchaguzi wa viongozi wa
kamati za Baraza la Vyama vya Siasa.
Wajumbe wa Baraza la Vyama vya
Siasa hutokana na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa, ambapo kila
chama cha siasa huwakilishwa na wajumbe wawili walioteuliwa na chama
husika. Baraza la vyama vya Siasa ndicho chombo maalumu cha kisheria
ambacho hutumiwa na vyama vya siasa kujadili masuala mtambuka ya
kisiasa.
No comments:
Post a Comment