SERIKALI Mkoani Tabora imewaagiza
viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) kutowapa makisio ya
kilo za kilimo cha tumbaku msimu ujao wakulima ambao watashindwa kupanda
miti kama Sheria na taratibu za kilimo cha zao hilo zinavyotaka ndani
ya msimu huu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
upandaji wa miti kupitia Vyama vya Msingi wa Ushirika na wanachama wao
ambao ni wakulima wa zao la tumbaku katika Wilaya ya Urambo na Kaliua.
Alisema kuwa Sheria zinawataka
wakulima wa tumbaku kupanda miti 250 kila mwaka kwa ekari moja lakini
wapo ambao kila mwaka wamekuwa hawapandi miti huku wakiendelea kuharibu
mistu kwa kukata miti ikiwemo asili.
Mwanri alisema kuwa vitendo cha
baadhi wakulima kukata miti bila kupanda vimeanza kusababisha baadhi ya
miti ya asili kama vile mninga, mkurungu na mingine ambayo inasoko kubwa
duniani kuwa hatarini kupoteza.
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika
Msingi cha Imalamakoye Ibrahimu Kagete alisema kuwa wanachama wa Chama
hicho wamenunua shamba lenye ukubwa wa ekari 100 ambazo wameanza kupanda
miti.
Alisema kuwa lengo la Chama hicho
ni kupanda miti katika ekari 10 kila mwaka ambapo hadi hivi sasa
wameshafikisha ekari 11 na kufikisha miti 11,000 ya aina mbalimbali.
Kagete aliongeza kuwa wanacha wa
Chama hicho wameshakwisha panda jumla ya miti 448,750 na kuongeza kuwa
wanafanya hivyo ili kuitia wito wa Serikali na Kampuni za kuwataka
kupanda miti kila mwaka kama njia ya kupata nishati ya kukwawishia
tumbaku.
Alisema kuwa wanatambua kuwa bila
kuwa hakuna miti hakuna tumbaku na hivyo wasipopanda miti wanaweza
kusababisha kilimo cha tumbaku kufa.
Naye Afisa Ushirika kutoka Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa Fortunatus Mkoba aliwataka viongozi wa Vyama vya
Ushirika Vya Msingi kuhakikisha mkulima ambaye hana bani la kisasa la
kukaushia tumbaku hasiruhusiwe kulima zao hilo.
Alisema kuwa haitakuwa na maana
kama watu wanapanda miti lakini mabani yanatumika katika kukaushia
tumbaku ni yale yale ya kizamani na ambayo yatumia magogo na kuni
nyingi.
No comments:
Post a Comment