California limekuwa jimbo kubwa zaidi nchini Marekani
kuhalalisha matumizi ya bangi kwa burudani.
Kuanzia sasa Januari mosi mwaka 2018 watu walio na umri wa
kuanzia miaka 21, wanaweza kumiliki hadi gramu 28 za bangi na kupanda hadi miti
6 ya bangi nyumbani.
Wanaopinga wanasema kuwa sheria hiyo itasababisha watu
kuendesha magari wakiwa tayari wamevuta bangi kuchangia vijana kuvuta bangi.
Lakini biashara zinatabiri kile kinaonekana kuwa sekta ya
mabilioni ya dola miaka michache inayokuja.
Wakaazi wa Califonria walipigaa kura kuunga mkono kipengee
cha kuhalalisha bangi miaka 14 iliyopita katika kura ambayo ilifanyika sambamba
na uchaguzi wa rais nchini humo.
Tangu wakati huo sheria ngumu zinazohusu kodi zimeandikwa
kudhibiti mauzo ya bangi.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ambayo inafuatilia soko la bangi
duniani alitabiri kuwa kutakuwa na kushuka kwa bei kwa mwaka wa kwanza au miaka
miwili.
Hata hivyo, faida ni kubwa katika jimbo hilo tajiri zaidi na
lenye watu wengi zaidi nchini Marekani.
Mwaka 1996, California lilikuw jimbo la kwanza kuhalalisha
bangi kwa matumizi ya matibabu.
Inakadiriwa kuwa soko la bangi haramu kwa sasa ni dola
milioni 5.1 na wakati itahalalishwa thamani yake itakuwa ya dola bilioni 5.8
itakapofikia mwaka 2021.
No comments:
Post a Comment