Mtu mmoja nchini Kenya mwenye umri wa miaka 35 amefikishwa mahakamani
akituhumiwa kubaka mbuzi wawili wa jirani yake, na kisha kuwaua.
Tukio hilo limetokea Januari 13 mwaka huu, baada ya watu kumuona
akiwaburuza mbuzi hao kutoka porini ambako anahisiwa kufanya tukio hilo,
katika eneo la Kangundo
Waendesha mashtaka wametaka mbuzi hao wapelekwe kufanyiwa vipimo ili
kubaini kama kweli wamefanyiwa kitendo hicho, na kutaka mshtakiwa
kupatiwa matibabu baada ya kulalamika alipigwa vibaya na polisi
walipoenda kumkamata.
Kesi hiyo imehairishwa mpaka Januari 29, na mshtakiwa kupewa dhamana ya shilingi 100,000 za Kenya.
Sheria za Kenya zinamtaka mtu atakayekutwa na hatia ya kufanya ukatili kama huo kwa wanyama kwenda jela kwa miaka 14.
No comments:
Post a Comment