Wananchi wa
kijiji cha msosa kilichopo tarafa ya Ruaha mbuyuni wameifukuza kamati yamipango
na fedha kwa tuhuma za kufanya ubadhilifu wa mali za kijiji na kuunda kamati
mpya itakayoleta maendeleo katika kijiji hicho.
Wakizungumza
wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho wananchi wameutaka uongozi
wa kamati hiyo kuachia ngazi kutokana na tuhuma zinazowakabili.
Kwa upande
wake mtendaji wa kata Maiko Chabili ameafiki kuvuliwa madaraka kwa viongozi wa
kamati ya mipangano na fedha hivyo kamati ya mipango na fedha ya kijiji cha
msosa wamekubali kujiuzuru na kulipa pesa ambazo wamezitumia vibaya bila ruhusa
ya wananchi.
No comments:
Post a Comment