Katika matatizo, huzuni na giza, tujifunze kutokana na
Mtakatifu Yosefu ambaye anatambua namna ya kutembea gizani, anavyosikiliza
sauti ya Mungu na kama anavyokwenda mbele kwa ukimya.
Huo ndiyo ushauri wa Baba Mtakatifu Francisko siku ya
Jumatatu 18 Desemba 2017 katika mahubiri yake kwenye Kanisa cha Mtakatifu
Martha mjini Vatican.
Ametafakari hayo akitazama Injili ya siku ya Mtakatifu
Matayo, ambayo inaeleza kuwa, juu ya uzao yaani, Yesu atazaliwa na Maria
mchumba wa Yosefu mwana wa Daudi.
Baba Mtakatifu akitafakari zaidi anaonesha mshituko wa
Yoseph, hasa Maria alipoanza kuwa na ishara za kuonesha ujauzito na zaidi
mara baada ya Maria kurudi kutoka kwa Elizabeth.
Ni wazi kuonesha wasiwasi wa mtu huyo katika uchungu na
mateso ya , kwa maana watu katika kijiji kile walianza maneno.
Na kwa upande wa Yosefu hakuwa na ulewa kama Maria alikuwa
mama wa Mungu na ndiyo maana aliamua kumwacha kwa kimya bila kumtangaza
kwa umma, hadi Bwana alipoingilia kati kwa njia ya malaika katika ndoto ambaye
alimweleza kuwa mtoto atakayezaliwa naye ni kwa njia ya Roho Mtakatifu na kwa
njia hiyo Yoseph aliamini na kutii.
Yoseph alipata mapambano ya ndani ya roho yake,
mapambano hayo yalikuwa na sauti ya Mungu, japokuwa sauti ile mara nyingi
ilikuwa ni mwanzo wa utume wake, kama isikikavyo mara kwa mara katika
Biblia, na ndiyo sauti ile ya “amka na umchukue Maria nyumbani mwako”.
Ilikuwa ni kumwakikishia juu ya wajibu wake katika hali hiyo; hali ambayo alitakiwa kuwa nayo mikononi mwake na kwenda mbele. Lakini Baba Mtakatifu anafafanua kwamba Yosefu hakwenda kwa marafiki kutafuta ushauri, hakwenda wa wataalam ili watafsri ndoto yake, yeye aliamini tu na kuendelea mbele.
Alichukua wajibu huo mikononi mwake. Lakini ni kitu gani
alitakiwa kuchukua mikononi mwake Yesefu? Hali yake ilikuwaje? Je Yosefu
alikuwa abeba nini ?Baba Mtakatifu ametoa jibu kwa, Yosefu alitakiwa
kuwajibika kwa mambo mawili: kwanza ubaba na ile ya fumbo! Nini maana ya kubeba
ubaba:
Anaongeza kusema,
yeye alitakiwa kubeba ubaba. Kwa maana ni kitu kilichotambulika tayari kwenye
uzao wa Yesu ambapo kama wanavyoeleza kwamba alikuwa ni mwana ya Yoseph. Yeye
alibeba mzigo, huo wa ubaba ambao haukuwa wake: kwa maana ulitokana na Baba.
Yeye alipeleka mbele
ubaba ukiwa na maana ya kwamba si katika kusaidia Maria na mtoto, bali hata kufanya
mtoto akuwe , kumfundisha kazi, hadi kumfikisha katika ukomavu wa kiume. Yosefu
alichukua jukumu la ubaba usiyo wa kwake, bali wa kutoka kwa Mungu na alibeba
bila kusema neno lolote.
Katika Injili zote hawasemi neno lolote lililotamkwa na
Yosefu. Ni mwanaume kimya na mtiifu wa ukimya. Yeye alichukua fumbo
mikononi mwake ili kuwapeleka watu wa Mungu, kama inavyoeleza katika somo la
kwanza kwamba, ni fumbo la kuwapeleka kwa Mungu, ni fumbo la uumbaji ambalo
liturujia inaonesha maajabu ya kazi ya uumbaji. Na ndiyo maana Yosefu alichukua
mikononi kwake fumbo hili na kusaidia kwa ukimya wake, katika kazi yake hadi
ilipotimia wakati wa kuitwa kwake na Mungu.
Mwanaume huyo Baba Mtakatifu anabaisha, alibeba ubaba na
fumbo, ambalo lilitwa kivuli cha Mungu Baba.
Na iwapo Yesu alijifunza kuita baba kwa baba yake,
aliyekuwa anamfahamu kama Mungu, ilitokana na kujifunza maisha kutokana na
ushuhuda wa Yosefu mwanaume ambaye alimlinda, mwanaume aliye mfanya akue na
mwanaume anayepeleka maana na kila fumbo lakini bila kuwa na lolote la
kwake.
Baba Mtakatifu amemalizia kwa kusema, Yosefu ni mtu mkubwa
ambaye Mungu alikuwa na haja naye ili aweze kupeleka fumba la kuwarudisha watu
wake kuelekea katika uumbaji mpya.
No comments:
Post a Comment