Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kadinali Pengo amewataka wakristo wote na watanzania kwa ujumla
kudumisha amani kwa sababu ni tunu inayoliliwa na mataifa yote ulimwenguni.
Amesema amani haiwezi kuja bure bali kila mtanzania anatakiwa
kufanya kazi inayompendeza Mungu usiku na mchana ndipo amani itapatikana.
Askofu Pengo ameyasema hayo katika siku ya Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Maurus
Kurasini jijini Dar es Salaam wakati akitoa salamu za Krismas ambapo alizaliwa
Mwokozi Yesu Kristo.
Amesema hakuna njia ya mkato ya kuleta na kudumisha amani
Tanzania na duniani kwa ujumla zaidi ya kufanya mambo yenye kumpendeza na
kumtukuza Mungu.
Amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuifanya nchi kuwa na amani
na mshikamano na amewataka watanzania kila mtu kwa imani yake kumwombea Rais
ili aendelee kuiongoza nchi katika maendeleo anayohitaji Mungu.
Aidha Askofu Pengo amesema kuwa anatambua juhudi zinazofanywa
na mataifa mbalimbali na watu mashuhuri kuleta amani duniani lakini
akawakumbusha watanzania kuwa ni bora amani inayojengwa na watanzania wenyewe
kuliko amani ya kuletewa.
Amesaema njia pekee ya kuwafanya watoto wetu waseme na Mungu
ni kupitia mafundisho kanisani hali inayowasaidia kumjua Mungu na yale yote
yanayompendeza na yale yote aliyokataza.
No comments:
Post a Comment