MOSHI
MUFTI wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir Bin Ally amesema
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Bakwata halitawavumilia wale wote wanaotumia
dini Kiislamu kueneza mafundisho yaliyo kinyume na maadili ya Uislamu.
Shehe Zubeir ametoa onyo hilo mwishoni mwa wiki mjini Moshi,
Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa madrasa na maktaba ya chuo cha
Izzadini, vilivyoko eneo la Njoro, Manispaa ya Moshi, ambapo pia alichukua
fursa hiyo kuwatakia Wakristu heri ya Sikukuu ya Krismasi.
Amesema siku zote Bakwata inasisitiza mafundisho ya kidini
yafanyike ili mradi watu wapate elimu kuanzia ngazi za chini na kwamba wale
watakaobainika kutumia nafasi hizo vibaya watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hata hivyo amesema Bakwata itaendelea kupiga vita fikra
potofu ambazo zimekuwa zikienezwa na mafundisho yanayolenga kuwaharibu Waislamu
hasa vijana ambao ndiyo nguzo ya Uislamu katika miaka ya baadaye.
No comments:
Post a Comment