Mchungaji Jeremia Mollel wa
kanisa la Tag Olmuringaringa ametoa bati
24 kwa waamini watatu wa kanisa hilo
ikiwa ni mwendelezo wa kanisa hilo kusaidia watu wasio jiweza wanao abudu ndani
ya kanisa hilo kila baada ya mwisho wa mwaka.
Zoezi hilo limefanyika katika
kanisa la TAG Olmuringaringa lililopo
wilayani Arumeru Mkoani Arusha nchini
Tanzania.
Mchungaji Jeremia Mollel amesema
wameamua kufanya hivyo ili kujiona hawa waamini nao pia ni sehemu ya jamii.
Aidha ametoa kiasi cha shilingi
laki tano kwa wanafunzi walio katika mazingira magumu zaidi ya ishirini wa shule za msingi na sekondari kwaajili ya
vifa vya shule na na manunuzi ya sale za
shule.
Kwa upanda wao baadhi ya waamini
ambao wamepewa bati hizo na fedha
wamemshukuru mchungaji huyu na kubainisha kuwa watazitumia
kwa malengo yaliyo kusudiwa.
Hata hivyo zaidi ya wajane 25
wamepewa gunia mbili za za mchele kwaajili ya kusheherekea sikuku ya krismasi
na Mwaka mpya.
Itakumbukwa kuwa kanisa la TAG olmuringa ni kanisa ambalo limekuwa likito fedha na vifaa mbalimbali kwa waamini kila mwisho
wa mwaka ikiwa ni njia moja yapo ya kuitangaza injili.
No comments:
Post a Comment