
Mpanda mijengo mirefu ambaye ni maarufu sana nchini China
amefariki akionyesha moja ya ujuzi wake hatari.
Wu Yongning alikuwa amejizolea maelfu ya mashabiki kwenye
mtandao ya kijamii wa Weibo, kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu
ya majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.
Wasi wasi uliwaingia mashabiki wake wakati aliacha kuchapisha
video zake mwezi Novemba.
Sasa imeibuka kuwa alikufa baada ya kuanguka kutoka jumba la
ghorofa 62 kwenye mji wa Changsha.
Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa alikuwa
akishiriki kwenye mchezo wa kushinda pesa nyingi.
No comments:
Post a Comment