Madereva nchini wamepongezwa
kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti katika kukabiliana
na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali pamoja na vifo
vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji unaofuata taratibu na sheria za
barabarani.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa
Kikosi cha Barabarani Tanzania Fotunatus Mselemu Kamishana Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi(SACP) wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa
kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani unaojumlisha
mashirika yasiyo ya Kiserikali
Kamanda Mselemu alisema tatizo
la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu wengi wanafariki na
kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani”sisi sote ni wahanga wa usalama
barabarani hivyo hatuna budi wadau wote kushirikiana katika
kukabiliana na suala hili na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili
usalama wa barabarani uimarike na kuboreka zaidi”Alisema.
Alisema hivi sasa watu wengi
wameanza kubadilika hususan madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi
jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza
kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa
salama wanapotumia vyombo vya moto
No comments:
Post a Comment