
Mwanamke ambaye alichukuliwa kutoka kwa mama yake baada ya
kuzaliwa nchini Argentina, ameunganishwa na familia yake na kundi
linalofahamika kama Grandmothers of the Plaza de Mayo.
Adriana, 40, ambaye alionba jina lake la pili kutofichuliwa
alitambulia baada ya kufanyiwa uchunguzi wa DNA.
DNA yake ililingana na ya familia ya wazazzi wake ambao
walitokeka wakati wa utawala wa kijeshi nchini Argentina.
Adriana ndiye mtoto wa 126 kupatwa na Grandmothers, ambao
wanaendesha kampeni kwa niaba ya waathiriria wa "Dirty War".
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari, Adriana
alisema kuwa wakati watu waliokuwa wamemlea walikufa, aliambiwa na mtu mwingine
kuwa yeye hakuwa mtoto wao wa kuzaliwa.
Alifanyiwa uchunguzi wa DNA na baada ya miezi minne hakupata
DNA iliyolingana na yake, kutoka kwa ile inayohifadhiwa na Grandmothers ya watu
walitoweka au kuuliwa na utawala wa kijeshi.
"Nilianza kufikiri kuwa nilitelekezwa, nilipeanwa au
kuuza kwa sababu hawakuwa wananitaka." alisema Adriana.
Lakini siku ya Jumatatu alipata simu kutoka tume ya kitaifa
ya haki ya kutambuliwa, ikimuambia kuwa walikuwa na ujumbe wangependa kumpa
yeye.
Adriana alienda mara moja na kuambiwa kuwa alikuwa binti wa
Violeta Ortolani na Edgardo Garnier, wote waliotoweka wakati wa utawala wa
kijeshi.
No comments:
Post a Comment