Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema wakati wa kuelekea sikukuu za Krismasi na mwisho wa mwaka, mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Mbeya, Songwe, rukwa na Kigoma.
Meneja wa kituo Kikuu cha Utabiri wa Hali ya Hewa wa TMA, SAmuel Mbuya,
alieleza kuwa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya ukanda wa
Pwani ni zile za kumalizika kwa msimu wa vuli.
Mkurugenzi Mbuya alieleza kuwa Mikoa hiyo minne iliyotajwa ndiyo
inayotarajiwa kuwa na mvua wakati wa sikukuu na ifikapo mwisho wa mwezi
huu, mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali ikiwamo Dar es
Salaam zitakuwa zimefikia ukingoni.
“Mvua zinazonyesha maeneo ya ukanda wa Pwani ni zile za vuli na zilianza
Oktoba na zinaisha mwisho wa mwezi huu, si mvua zinazoendelea isipokuwa
tu katika mikoa ya Mbeya, Songwe Rukwa na Kigoma ambako katika msimu
huu wa sikukuu kutakuwa na mvua,” alisema.
Aliongeza kuwa TMA inatarajia mvua zitaendele kunyesha katika mikoa ya.
Kigoma, tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Dodoma na
Singida. Alisema mvua katika mikoa hiyo zilianza kunyesha Novemba na
zinatarajiwakumalizika mwezi Aprili.
Mbuya aliwataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na
TMA mara kwa mara, ili kupata mwelekeo wa hali ya hewa pamoja na
kuchukua tahadhari mapema.
No comments:
Post a Comment