Kijana Msigala Salum amekatwa
masikio yote mawili baada ya kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitatu katika
eneo la Majengo Mapya mkoani Shinyanga.
Taarifa zinasema Kijana huyo mwenye
umri wa miaka 24 alitenda kosa hilo Disemba 20,2017 majira ya saa tatu asubuhi.
Kijana huyo anayejishughulisha na
shughuli ya kuosha magari mkazi wa Ndala alimdanganya mtoto huyo wakati
akicheza na wenzake nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio
hilo wamesema kutokana na tukio hilo mtuhumiwa alishambuliwa na wananchi kabla
ya jeshi la polisi kufika.
Aidha akitoa taarifa kwa vyombo vya
habari leo Alhamis Desemba 21,2017 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga
ACP Simon Haule alisema jeshi hilo linamshikilia Msigala Salum.
Hatahivyo Kamanda Haule amesema mara baada ya
tukio hilo baba mzazi wa mtoto alimkamata mtuhumiwa na kumkata masikio yote
mawili kwa kutumia kisu na kukimbia.
No comments:
Post a Comment