
Mji mdogo wa Minas nchini Uruguay umeweka rekodi kwenye
kumbukumbu ya Guinness kwa kuandaa shughuli kubwa ziadi duniani ya kuchoma
nyama.
Karibu wapishi 200 walitumia tani 60 za kuni kuwasha moto
mkubwa ambapo tani 16.5 za nyama iliyochomwa kwa muda wa jumla ya saa 14.
Lengo lilikuwa ni kubuni rekodi ya awalia ya Argentina ambayo
ilichukua rekodi kutoka Uruguay mwaka 2011

Kuna ushindani mkali kati ya mataifa hayo mawili jirani
kuhusu ni nani anazalisha nyama bora.
Uruguay iliyo na ng'ombe mara tatu zaidi kuliko idadi ya
wakaazi wake ni moja ya wauza wakubwa wa nyama duniani.
Nyama iliyovunja rekodi ilipimwa mara mbili, kwanza ikiwa
mbichi na pili baada ya kuchomwa.
Nyama iliyochomwa ilistahili kupiku ile ya tani 9.16
iliyochomwa kwenye mji wa Pampa nchini Argentina mwaka 2008.
Iliripoitiwa kuwa nyama hiyo ya Uruguay ilikuwa ya tani
10.36.
Waandalizi wanasema kuwa maelfu ya watu walikusanyika
kutazama shulghuli hiyo na kula nyama.

No comments:
Post a Comment