KILIMANJARO
Katika hali isiyokua
ya kawaida mkutano wa kuchagua viongozi wa chama cha ushirika mashua wilayani
Hai mkoni kilimanjaro umevunjika baada ya majina ya baadhi ya wagombea
kutoonekana.
Mkutano huo uliokuwa
ufanyike katika ofisi ya Kijiji cha Mashua kwa lengo la kuchagua viongozi mbali
mbali wapya wa chama hicho akiwamo mwenyekiti wa chama.
Wakizungumza wanachama
wa chama hicho cha ushirika cha mshua mara baada ya uchaguzi huo kuvurugika
Angel George na Samson Mmari wamesema uchaguzi huo haujazingatia vigezo
kutokana na kukosa baadhi ya majina ya waliowapitisha.
Kufuatia changamoto
hiyo wamemuomba mrajisi wa ngazi ya Taifa Tito Haule kuingilia kati jambo hilo ili uchaguzi ufanyika kwa
haki.
Kwa upande wake Afisa
ushirika wa wilaya hiyo ya Hai akiongea kwa njia ya simu amesema kuwa katika
kuchagua majina kamati inapitia majina kama mgombea hana sifa jina huondolewa
hivyo kutokana na hali hiyo wataandaa tena upya uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment