MKURUGENZI wa Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amemaliza hofu ya kuhamishwa iliyokuwa
imetanda kwa wafanyabiasha takribani 2,500 wa Soko la Sabasaba Mjini
Dodoma baada ya kuwahakikishia kuwa wataendelea kufanya shughuli zao
katika Soko hilo linalomilikiwa na Manispaa ya Dodoma na kwamba hakuna
wa kuwahamisha.
Aliyasema hayo jana alipofanya
ziara Sokoni hapo na kufanya mkutano na Wafanyabiashara hao ambao
walimueleza Mkurungenzi huyo kuwa wamekuwa wakipata taarifa zisizo rasmi
kuwa upo mpango wa wao kuhamishwa katika soko hilo hali inayowakosesha
usingizi na kutojua hatma yao.
“Hakuna kuhama hapa
ng’oo…Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ndiyo mmiliki wa Soko hili
ambalo asili yake hapo awali lilikuwa eneo la Maonesho ya Sabasaba
ambapo wadau mbalimbali walikuwa na vibanda vyao vya maenesho”
alifafanua Kunambi huku akishangiliwa na wafayabiashara hao.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Kunambi alifuatana na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede.
Wafanyabiashara hao waliishukuru
Manispaa ya Dodoma baada ya viongozi hao kufika na kuzungumza nao katika
wakati muafaka baada ya kufanya biashara zao kwa wasiwasi mkubwa kwa
siku kadhaa.
No comments:
Post a Comment