Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga
linawashikilia watu sita wakiwemo raia wanne wa China kwa kosa la
kusafirisha na kuhifadhi mawe yanayosadikiwa kuwa na madini kinyume cha
sheria.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Simon Haule
watuhumiwa walikamatwa Disemba 6,2017 saa saba mchana katika kata ya
Ibadakuli wilaya ya Shinyanga na askari wa usalama barabarani wakati
wakikagua roli lenye namba za usajili T 209 AVH lililokuwa limebeba mawe
hayo yaliyochongwa mfano wa virungu.
Kamanda Haule alisema baada ya kuwakamata wachina hao na madereva wao,
walisema mawe hayo wanayapeleka kuyahifadhi kwenye kwenye kiwanda cha
kutengeneza mafuta ya kula cha Jielong Tz Co . Ltd kilichopo mjini
Shinyanga.
Raia wa China waliokamatwa ni Bai Tao 40, Chen Dunlu 33, Huanran Liu na
Jianhua Xiong na madereva wao wawili ambao ni Anwari Shabani na Joseph
Kapoli.
Mmiliki wa mali hizo Huanran Liu amekiri kutokuwa na lesseni wala kibali
cha kusafirisha mawe hayo na kudai yeye ni mtafiti wa madini na
ameyahifadhi kwenye kiwanda hicho cha mafuta kwa muda tu
No comments:
Post a Comment