Watanzania
wameelezwa kuwa wanyenyekevu katika matendo yao ya kila siku hapa
duniani wakati wakiwajibika kwenye shughuli zao za kila siku kwa kutenda
kazi zao kwa uadilifu kwani jukumu lao kuu ni kutambua na kutengeneza
njia ya muumba.
Hayo
yamesemwa na Padri wa Kanisa la Roho mtakatifu wilayani Hapa Festo
Lubuva wakati wa misa ya shukrani na kuwataka kuendeleza kuwaombea
viongozi wetu wakati huu wa ibada ya kuzaliwa kwa Kristo.
Padri
Lubuva amewaambia waumini hao walioshiriki ibada hiyo kuwa jukumu la
kila mmoja wetu hapa duniani ni kutengeneza njia ya bwana na mungu hivyo
yampasa kila mmoja wetu kujiuliza kama kweli amesimama imara kwenye
njia hiyo.
“Nadhani
ifike mahali tukawa tuajiuliza kama wangapi tumeipokea na tukayafanyia
kazi yale yote yanayotupasa kuyafanya katika kuhakikisha tumesimama
kwenye njia ya bwana” alisisitiza Padri Lubava.
Amesema
kuwa watanzania bila kujali itikadi zetu tunatakiwa kujiuliza malengo
yetu ya kuja hapa duniani je hatutendi dhambi na kuwa kila mmoja wetu
akijichunguza na kujiona anafuata malengo hayo atajikuta hatendi
yamchukizao bwana na nchi yetu itaendelea kubarikiwa.
Amsema
kuwa kama tunavyomuombea leo mama yetu hapa yeye alitiumiza kwa nafasi
yake hivyo wajibu wetu nasi kutimiza yale yampendezayo mungu na
kuhakikisha wajibu wetu kwa jamii inayotuzunguka tunatekeleza bila
kungoja kusukumwa wala kufanya ufisadi wa mali za umma.
Aidha
Nawaomba watendaji wote wa serikali kuhakikisha wanatekeleza majukumu
yao kwa uadilifu wakati huu wa sikukuu ya Xmas kujitoa kama walivyofanya
bwana wetu yesu kristo ili kila mmoja afaidi maisha ya kuwa hapa
duniani.
“Nawasihii
watanzania kufanyakazi kama maandiko yanavyosema lengo likiwa ni
kufikia malengo tuliojiwekea ya kufikia uchumi wa kati wa viwanda na
kuweza kuondoa ombwe
No comments:
Post a Comment