Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa siku kumi kwa jengo la
Tanesco lililopo Ubungo libomolewe ili kupisha ujenzi wa barabara ya
Morogoro.
Waziri huyo pia amewataka watumishi wa Tanesco wanaosimamia jengo hilo
na wakandarasi waliowekwa kubomoa jengo hilo wasisafiri wala kusherekea
Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya bali washughulikie jengo hilo
kuvunjwa.
“Nataka kuanzia leo Desemba 22 ndani ya siku sita jengo hili lote
libomoke na kwasababu ni majengo mawili ndani ya siku kumi majengo yote
mawili yawe yamebomoka kama mnaona vigumu kubomoa jengo lenu waambieni
TBL ”amesema
Amesema hadi kufikia mwisho wa mwezi huu jengo hilo lote liwe
limeanguka chini na hakuna cha sikukuu wala Krisimasi kwenye kubomoa
jengo hili na ujenzi wa barabara kama Tanesco wanaaza waanze
tusiwakwamishe”amesema.
Amesema wananchi wameshabomoa majengo yao kwanini Tanesco bado
wanasuasua na kudai Januari mosi ataenda tena kukagua kuona kama agizo
lake limefanyiwa kazi.
“Naimani wananchi hawatapata shida wakati wa sikukuu ya Krismasi na
mwaka mpya ,kwa hiyo asiruhusiwe mtumishi yoyote wa Tanesco kwenda nje
ya ofisi yake wakati wa sikukuu zote mbili”amesema
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Kahitwa Bishaija amesema
wamelisikia agizo la Waziri na wataenda kulitekeleza kama lilivyo.
No comments:
Post a Comment