MUME wa mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Nigeria, Osinachi Nwachukwu aliyefariki dunia Ijumaa katika hospitali jijini Abuja, amekamatwa na polisi kufuatia madai yanayoendelea kusambaa kwamba alihusika na kifo chake kwa kumpiga na kumjeruhi vibaya mwimbaji huyo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi la Nigeria, amenukuliwa na tovuti za Daily Trust and Punch akithibitisha kukamatwa kwa Peter Nwachukwu baada ya malalamiko kutoka kwa kaka wa mwimbaji huyo anayedai kwamba ndugu yake aliuawa na mumewe.
Osinachi alipata umaarufu 2017 baada ya kuimba wimbo wa injili uitwao Ekwueme alioshirikiana na Prospa Ochimana.
No comments:
Post a Comment