Jeshi la Israel limesema kuwa Wapalestina wamechoma moto madhabahu yanayothaminiwa na Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi, wakati majeshi ya Israel yakiendesha operesheni katika eneo hilo kufuatia mfululizo wa mashambulizi ya hivi karibuni yanayofanywa na Wapalestina nchini Israel.
Eneo lililohujumiwa linafahamika kwa wayahudi kama kaburi la Joseph na limekuwa kitovu cha mvutano mkubwa kati ya jamii hiyo na waislamu.
Hayo yanajiri wakati mvutano kati ya Waisraeli na Wapalestina umekuwa mkali hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ambao mwaka huu umeingiliana na sikukuu kuu za Kiyahudi na Kikristo.
No comments:
Post a Comment