Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Utalii Kutoka Chuo cha Taifa
cha Utalii Kamapas ya Arusha wametakiwa kuwa wazalendo Waaminifu na Waadilifu
ili kujenga Taifa la watu wenye waledi na Uchumi Mzuri.
Hayo Yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Athumani
Kihamia wakati wa Hafla ya Wahitimu wa Mafunzo Maalum katika Chuo cha Utalii Kampasi ya Arusha
Yaliyodhaminiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, vijana na Wenye Ulemavu.
Naye Meneja wa Chuo hicho Dr. Maswet Masinda Ameiomba Serikali
Chini ya Rais Samia Suluhu Hasani Kuendelea Kufadhili Wanfunzi Mbalimbali wenye
Uhitaji ili kutengeneza ajira kwa Vijana na kuwafanya Kujitegemea.
Baadhi ya Wanafunzi walio Hitimu Mafunzo hayo wameishukuru
ofisi ya wazri Mkuu kwa Kufadhili Mafunzo Haya kwani wameweza Kupata ajira Kazi
kupitia Kozi Walizo Soma.
Zaidi ya Wanafunzi 111 Wamehitimu Mafunzo haya Maalum Yaliyodhaminiwa
na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, vijana na Wenye Ulemavu kutoka Mikoa
Mbalimbali Nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment