Mamlaka ya Maji Jiji la
Arusha (AUWSA) wametoa ofa kwa wale watumijia wa maji ambao wamesitishiwa
huduma kuwa wafike katika ofisi za kanda ili waweze kurejeshewa huduma za Maji.
Hayo yamesemwa na Afisa
Mahusiano Msaidizi Anny Mshana Kutoka Mmamlaka ya Maji Jijini la Arusha (AUWSA)
Katika Kipindi cha Amka Uangaze Kinachopeperushwa kila asubuhi Habari Maalum fm.
Anny amesema Mteja Baada ya Kufika
Katika Ofisi Hizo ataeleza changamoto
zake na Kupewa Mkataba ambao Utamuelekeza kulipia kidogo kidogo huku akiwa wanatumia
maji kama kawaida.
Amebainisha kuwa ofa hiyo ni Mwisho Mwezi
March 31,2022 kwa wateja wote ambao wamesitishiwa huduma kwa namna moja ama
nyingine ili waweze tena kufurahia huduma ya maji.
“iwapo mteja atachelewa
kufika katika ofisi zetu wakati wa kipindi hiki cha maji atatakiwa kulipia
faini ili aweze kurudishiwa huduma hio ya maji kwa sababu ofa inaisha tarehe March 31,2022 ”
Amesema Afsa Mshana.
Amesema kuna wateja ambao wamesitishiwa huduma
kwasababu ya kushindwa kulipia bili za maji wanatakiwa wafike kwenye ofisi za
kanda na nusu ya kiasi wanachodaiwa ili waweze kurudishiwa huduma na kuendekea
kulipia kidogo kidogo kwa deni lililobakia.
“Mtu anatakiwa awe na nusu
ya kiasi anachodaiwa naafike kwenye ofisi zetu apewe namba ya kulipia maji na
siku hio hio atafunguliwa huduma nakuendelea kufurahia hio ndio ofa kabambe”
Amesema Mshana.
Hata hivyo Afisa huyo
amesema kuwa mbali na huduma ya maji wanatoa mafunzo mbalimbali ya utuzaji wa
mazingira kwa wanafunzi walioko mashuleni na namna ya kutunza vyazo vya maji.
No comments:
Post a Comment