WAZIRI wa Maji Jumaa Awesso, amekagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Maji wa Namanga Mkoani Arusha ambao hivi sasa ujenzi wake umefika asilimia 92.
Mradi huo chanzo chake ni mto Simba uliopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, na utahudumia mji wote wa Namanga pamoja na kata ya Kimokowa ambapo ni eneo ambalo mradi huo unapita.
Aweso amesema utekelezaji wa mradi huo ni mahsusi katika kuhakikisha ahadi, maagizo na maelekezo aliyotoa Rais Samia Suluhu, Oktoba 18, 2021 akizindua mradi mkubwa wa maji wa Longido wenye thamani ya Sh. bilioni 15.7 katika Wilaya ya Longido, ambapo alimuagiza Waziri huyo wa Maji kuhakikisha mji wa Namanga unapata maji ya uhakika safi na salama.
No comments:
Post a Comment