Kwaya ya mtakatifu Cesilia Yenye Makao yake Makuu Mkoani Arusha Mwishoni mwa Wiki Lilopita Imefanikiwa kufanya Ibada ya kumshukuru Mungu Baada ya Kuibuka Kidedea katika Utoaji wa Mirabaha kwa Mara ya Kwanza Nchini Tanzania.
Ibada hiyo ya Shukrani iliambatana na Tamasha la Uimbaji lililoandaliwa na Kwaya Hiyo katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Mtoto Yesu Jimbo Kuu la Arusha.
Mgeni Rasmi katika Tukio hilo Askofu msaidizi Jimbo kuu Katoliki Mkoani Arusha Muhasham Prosper Limo amesema kuwa amefurahishwa na tukio hilo la kwaya ya Mt Cesilia Kuwa Kinara kwa Mara ya Kwanza baada Serikali ya Tanzania kuanza Kulipa wasanii kwa kupokea mrabahamkubwa kwani kwaya ni utumishi wa kusambaza neno la Mungu.
Makamu Mwenyekiti wa kwaya hiyo Bi Bertha Gerald John amesema wanamshukuru sana Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan kwa kutambua wasanii au vikundi mbalimbali vya uumbaji hapa Nchini.
Aidha Mlezi wa kwaya ya Mtakatifu Cesilia Bi Dinna Patrick amesema kuwa kwaya hiyo imedumu takribani miaka 77 iliyopita na kilichochangia kuwa hivyo ni maombi na ushirikiano mkubwa kwa wanakwaya hao.
Hata hivyo Askofu Prosper Limo ametoa ushauri kwa wanakwaya hao kuendelea kuwa na umoja katika kila hatua kwa sababu kumuimbia Mungu kuna faida.
No comments:
Post a Comment