Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Connerstone Church lililopo Murieti Mkoani Arusha Mchungaji Dorcas Mbuya amesema Nguvu ambazo amekuwa akizitumia Kuponya na kuwambea watu ni Nguvu Halisi za Mungu Tofauti na Baadhi ya Watu wanavyo fikiria.
Mchungaji Dorcas ambaye Pia amekuwa akitumiwa na Mungu kwa Kuhudumia Mikoa Mbalimbali ndani na Nje ya Nchi Ikiwemo Kenya na Burundi kwa kuitwa na Watu kwajili ya Kuombea baada ya watu Kushuhudia shuhuda ambazo Mungu amekuwa akizifanya kwa Kumtumia maeneo Mbalimbali.
Akizungumza katika Kipindi cha Top Ten Ambacho Kimekuwa Kikiperushwa na Habari Maalum Fm Mchungaji Dorcas amesema kumekuwepo na Wachungaji ambao wamekuwa hawaamini kuhusu Nguvu za Mungu lakini Kwangu Mimi hizi ni Nguvu za Kweli za Mungu.
Akibainisha kuhusu Shuhuda Kubwa ambazo Mungu amemtumia Kuzifanya kwa watu ni Pamoja na Kumuombea Mwanamke Mmoja Jina Linahifadhiwa kutoka Mkoani Dodoma ambaye alikuwa amepoteza Mimba Mara Tatu lakini Baada ya Kumuombea alijifungua Mtoto wa Kiume.
“Nakumbuka Siku hiyo Baada ya Kujifungua alikuwa haamini Kabisa baada ya Mtoto Kulia alimwambia Mkunga achukue simu Yangu na atafute Jina Langu na Baada ya Hapo alinipigia na Baada ya Hapo alinitaka Nimuombee ili mtoto asife Nilimtaka asiwe na Hofu nilimuombea na Mpaka Hivi Sasa Mtoto ni Mzima Kabisa anaishi” Alisema Mchungaji Dorcas Mbuya.
Aidha Mchungaji Dorcass ambaye amekuwa akifanya Huduma ya Kitume kwa kwenda sehemu Mbalimbali ndani na Nje ya Nchi anapohitajika kwaajili ya Kutoa Huduma ya Maombi ya kwa watu wenye Mahitaji amesema Ushuhuda Mwingine aliwai Omba Kwaajili ya Bibi Mmoja ambaye alikuwa hajawahi washa Taa ya Chumbani Kwake Nyakati za Usiku na Hata Mchna Tangu alipo Hamia katika Nyumba ya Mtoto Wake na Baada ya Maombi Taa iliwashwa na Baada ya Kuwashwa kuliku na Nyoka ambaye alikufa Baada ya Maombi.
Hata hivyo Mchungaji Dorcas amebainisha kuwa Mungu Bado yupo enzini Licha ya Kuwa Baadhi ya wakristo wamekuwa hawaamini zile shuhuda ambazo wamekuwa wakiziona na Kuzisikia lakini hawana Budi Kuamini.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Mchngaji Dorcas Mbuya
Huduma : Mchungaji Kiongozi
Mahali : Arusha |Muriti
Kanisa : Conner Stone Church
Contact : +255716009361
No comments:
Post a Comment