Baada ya Account ya Instagram ya Mtangazaji na Mwandishi wa Habari za Kikristu Kutoka Upendo Media John Pazia kudukuliwa imerejeshwa kufuatia jitihada ambazo zimefanywa na IT Wake ili kuhakikisha kuwa account hiyo inakuwa salama na kuendelea kutoa taarifa za Injili.
Account Hiyo ambayo Ilidukuliwa siku ya Ijumaa ya Wiki Iliyopita Kuamkia Jumamosi Ilichukuwa siku Nzima Kuirudisha.
Akizungumza katika Kipindi cha Top Ten Ya Habari Maalum fm John Pazia mmiliki wa Instagram Account hiyo amesema Kazi za Kuchapisha Maudhui zinaendelea baada ya kadhia Hiyo Kufanyiwa kazi.
Akibainisha upatikanaji wa instagram account hiyo amesema kuwa IT Wake Ndio walifanikisha zoezi Hilo baada ya kupewa taarifa za kudukuliwa kwa account ya John Pazia.
“ Nilipo wapa taarifa watu wa IT wakanambia ngoja tuone tunafanyaje tukaendelea kuhangaika na marafiki zangu wakawa wananipa ushauri kuwa fanya hiki fanya hiki tunamshukuru Mungu maana kama lisaa limoja lililopita tulifanikiwa kuirejesha”Amesema John Pazia.
Aidha amebainisha kuwa pamoja na kudukuliwa kwa account yake sio kwamba alitumia mtandao vibaya maana hakupata ujumbe wowote kumjulisha kuwa ametuma taarifa ambazo sio za kwake au hazifai kwenye account hiyo.
“Kwenye instagram kama ni copy ya mtu mwingine huwa wanakupa ujumbe kuwa hii kazi niya mtu mwingine kwahio iondoe lakini mimi sijakutana na ujumbe wowote wakunitaarifu chochote “Amesema Pazia.
Hata hivyo John Pazia amesema kuwa anawashukuru sana watanzania kwa kufuatilia kazi zake kupitia mtandao wa instagram na facebook kwa kupatoa ushirikiano mzuri anajisikia furaha sana .
No comments:
Post a Comment