Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis  amekitembelea kwa mara nyingine kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki eneo ambalo lilikuwa kitovu cha wimbi la wahamiaji miaka 6 iliyopita na kuitaja tabia ya kuwapuuza wahamiaji kuwa ni "kwenda mrama kwa ustaarabu" duniani.

Papa Francis ambaye alitumia muda wa saa mbili kukizuru kisiwa hicho chenye kiasi waomba hifadhi 2,200 ameonya kuwa bahari ya Mediterrania inageuka kuwa eneo la makaburi lisilo na mawe na ulimwengu haujabadilika vya kutosha linapokuja suala la uhamiaji.

Akizungumza katika kambi ya wakimbizi ya Mavrovouni kisiwani hapo, kiongozi huyo wa kanisa Katoliki alisema "Barani Ulaya kuna wale wanaosisitiza katika kulishughulikia tatizo hilo kuwa suala lisilowahusu."

Papa Francis amesema sababu za msingi zinapaswa kushughulikiwa – siko watu maskini wanaolipigia gharama za mzozo huo na hata kutumika kwa propaganda za kisiasa.

 Ziara yake kwenye kisiwa hicho ni sehemu ya ziara yake ya siku tano nchini Cyprus na Ugiriki na imefanyika siku moja tangu alipotoa mataashi makali ya kukemea siasa za kizalendo alizosema zinatishia ustawi na demokrasia barani Ulaya

PAPA AKUTANA NA WAHAMIAJI KISIWANI LESBOS

No comments:

Post a Comment