Waumini
Wa Dini Ya Kikristo Duniani Wametakiwa Kuwa Na Akili Za Moyoni Badala Ya Kuwa Na
Akili Za Kibinadamu Pekee Ili Kuwa Na Uwezo Wa Kutumia Ufahamu Wa Kimungu Katika
Maisha Yao Ya Kila Siku.
Hayo Yamesemwa Na Mchungaji Kiongozi Wa Kanisa La Pentecoste Jerusalem Mpya Mchungaji Liberty Shirima Lililopo Kijenge Mwanamana Mkoani Arusha Wakati Wa Ibada Ya Jumapili.
Mchungaji Shirima Amesema Kuna Tofauti Ya Kiutendaji Kati Ya Akili Ya Kibinadamu Na Akili Ya Moyoni Kwani Akili Ya Kibinadamu Inafahamu Zaidi Mambo Ya Mwilini Na Akili Ya Moyoni Inafahamu Zaidi Mambo Ya Rohoni.
Aidha Amebainisha Kuwa Akili Ya Kichwani Inafahamu Zaidi Mambo Ya Duniani Tofauti Na Akili Ya Moyoni Inafahamu Zaidi Mambo Ya Ulimwengu Wa Roho.
Amesema Kuwa Kila Mwanadamu Ameumbiwa Akili Za Moyoni Lakini Baadhi Ya Wakristo Wameshindwa Kuzitumia Kwa Sababu Ya Kukosa Maarifa Ya Jinsi Ya Kuzitumia Ikiwemo Kusoma Neno Na Kumtafuta Mungu Katika Maombi.
“Ayubu Alipitia Jaribu Gumu Sana Hadi Mke Wa Ayubu Alimtaka Amkufuru Mungu Akafe Lakini Kilicho Msaidia Ayubu Ni Akili Ya Moyoni” Mchungaji Shirima.
Saul Petro Ni Mshirika Katika Kanisa La Pentecoste Jerusalem Mpya Anasema Mtu Akiwa Na Akili Ya Moyoni Mungu Anakuwa Karibu Zaidi Na Mtu Huyu Tofati Na Mtu Anaye Tumia Akili Ya Kibinadamu Peke Yake.
Kanisa La Pentecoste Jerusalm Mpya Lina Zaidi Ya Washirika 800 Linapatikana Kijenge Mwanama Kusini Mwa Mkoa Wa Arusha Likiwa Na Matawi Mbalimbali Nchini Tanzania
CHANZO CHA HABARI
Mchhungaji : Liberty Shirima
Contact : +25575364561
Kanisa : Pentecoste Jerusalem Mpya
No comments:
Post a Comment