Taasisi zinazojihusisha na Mradi wa EWAbelt ili kuboresha Mazingira, Kilimo na Ufugaji nchini Tanzania zakutana kujadili jinsi mradi utakavyo fanya kazi katika maeneo ambayo yametengwa ili Kutumia Mazao asili naKurudisha rutuba iliyo Potea katika udongo.
Akizungumza katika Mkutano uliofanyika Ofisi za Taasisi Inayo husiana na Utafiti wa Mazao (Tari Selian ) Kanda ya kasikazini Mratibu wa Mradi huo wa EWAbelt Profesa Kelvin Mtei kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela amesema Mradio huu unaratibiwa na Taasisi tatu kikiwemo Chuo Kikuu cha Mandela, Taasisi ya Tafiti za Mazao ya Kilimo Tari Selian Pamoja na Taasisi ya Kimataifa ya ICRAF.
Profesa Mtei amebainisha kuwa Mradiwa EWABelt Unafanyika Ukanda wa Kaskazini katika wilaya za Monduli, Meru na Same Dhumuni likiwa ni Kuboresha Kilimo na Ufugaji kwa kutumia Mbinu za Kisasa kutoka kwa wataalamu wa nchi za Mgharibi ambao wamebobea.
Aidha amebainisha kuwa Mradi huu wa EWABelt utasimamia na Kufanyia Mambo Makuu Matatu moja ikiwa ni Mmmonyoko wa Udongo, Mbili Kuangalia Mazao ya asili Yaliyo sahaulika na Tatu ni Matumizi ya zao la Ngwala kwa wakulima ili Kurutubisha Udongo.
Leon Mroso Kutoka Tari Makao Makuu Dodoma ambaye alifika Kwa Minajaili ya Kufungua Mkutano huo amesema mradi huu utasaidia Kurudisha rutuba ya udongo iliyo potea ambayo imepotea kwa sababu ya shughuli mbalimbali za Binadamu ikiwemo kilimo kisicho kuwa Rafiki kwa Ardhi.
Hata hivyo Msimamizi wa Mradi huo katika Taasisi ya Tari Selian Mtafiti Deodatusi Kiliba amesema waliamua kuitisha wadau mbalimbali wa kilimo na ufugaji ili kuwapa Mapokeo kuhusu Mradi huo ambao ulianza kufanya kazi Tangu mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment