Vatican City, Holy See (AFP). 

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amesema kupata chanjo ya kujikinga na virusi vya corona "ni kitendo cha pendo", wakati kiongozi huyo wa kiroho alipoungana na kampeni ya kuzidisha kujiamini kwa kupata kinga hiyo.

"Asante Mungu na kwa kazi ya wengi, sasa tunayo chanjo ya kutulinda dhidi ya Covid-19," alisema Francis katika ujumbe alioutoa kwa kampeni inayoongozwa na taasisi ya Marekani ya "It's Up to You (Ni uamuzi wako)".

"Wanatupa matumaini ya kumaliza janga hili, lakini kama tu itapatikana kwa wote na kama tukifanya kazi pamoja," alisema katika video, akiwa na ujumbe unaolenga jamii ambazo zimeathiriwa na virusi Kaskazini, Kati na Amerika Kusini.

"Kuchanjwa... ni kitendo cha pendo," alisema kiongozi huyo mwenye miaka 84.

"Na kuchangia ili kuhakikisha watu wengi wanachanjwa ni kitendo cha upendo. Kujopenda, kupenda familia na marafiki, kupenda watu wote".

Virusi vya corona vimeua angalau watu milioni 4.4 tangu mlipuko utokee nchini China Desemba mwaka 2019, kwa mujibu w atakwimu zilizojumlishwa na AFP.

Licha ya kampeni kubwa, dhana potofu na baadhi ya serikali au kampuni za dawa kutoamini zinachochea kusambaa kwa virusi.
 
Nchini Marekani, maeneo yaliyoathirika sana kwa kuangalia vifo vya Covid-19, sehemu kubwa ya vifo na maambukizi makubwa inahusu watu wasiochanjwa.

PAPA ASEMA KUCHANJA NI KITENDO CHA PENDO

No comments:

Post a Comment