Serengeti.
Watu wenye madaraka mbalimbali wameombwa kuacha tabia ya kuwakandamiza wenzao kwa uongo ili kujipatia rushwa.
Akihubiri katika misa ya Jumatatu ya Pasaka, Paroko wa Kanisa Katoliki Mugumu Jimbo Katoliki la Musoma, Padri Joel Marwa amesema matendo hayo yanakinzana na mpango wa Mungu ambaye anataka watu watawale kwa haki.
"Yesu alipofufuka walinzi walisema uongo kuwa wanafunzi wake wamemuiba wakati wao wamelala, lakini wanawake watatu waliofika kaburini waliendelea kusema ukweli bila kuogopa kuwa wamekuta kaburi wazi na Yesu alifufuka," amesema.
Amesema Maria, Salome na Magdalena wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi
hapa nchini kwa kuwa walisema ukweli ambao leo unatamalaki duniani hapa.
"Wanawake hawa ni viongozi tosha wanaotoa somo kwa viongozi mbalimbali hapa nchini maana hawakuogopa wayahudi, naomba sana walio na dhamana za uongozi watende kama hao wanawake," amesema.
Hata Hivyo amekemea sana dhuluma zinazofanywa na watu wachache waliopewa dhamana na kueleza wanasababisha migogoro na manung'uniko kwa jamii.
No comments:
Post a Comment