Dar es Salaam. 

Wakristo nchini wametakiwa kuacha kuishi maisha ya unafiki kwa utamaduni wa kuonekana wakiabudu kanisani mara kadhaa wakati maisha yao nje ya  uhalisia na tafsiri ya ukristo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani(DMP) kupitia ibada ya Pasaka leo Jumapili Aprili 4,2021 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), usharika wa Azania Front Jijini Dar es Salaam.

Kila mwaka mamilioni ya Wakristo duniani huadhimisha sikukuu ya kufufuka kwa Yesu Kristo aliyeuawa msalabani na kufanyika sadaka ili kukomboa wanadamu kupitia dhambi zao.
Katika ufafanuzi wake, Askofu Malasusa ametolea mfano wa msharika wake aliyemtembelea ofisini kwake na kukuta sifa mbaya juu yake.

Dk Malasusa amesema msharika huyo ambaye Jina linahifadhiwa  alikuwa ni bosi lakini wafanyakazi wenzake hawaoni uhalisia wa maisha yake ya ukristo.

“Kumbe matendo yake pale hayana ushuhuda, aliponiona akaanza kunawa mikono “bwana Yesu asifiwe Baba Askofu.Kwa hiyo haina maana tukiendelea kutenda maovu.”

Dk Malasusa amewataka watanzania kwa ujumla kuwa mabalozi wa matendo mema, kusambaza upendo na kutakiana kheri wakati wote ikiwa ni tafsiri halisi ya maisha ya ufufuko wa Yesu Kristo.

Wakati huo huo, amesema ufufuko wa Yesu kristo unatakiwa kubeba matumaini katika kipindi kigumu cha Maombolezo ya kitaifa na changamoto ya virusi vya corona.

ASKOFU MALASUSA AWAFUNDA WAKRISTO TANZANIA

No comments:

Post a Comment