Dar es Salaam.
Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Padre Alista Makubi amesema watu bado wanang'ang'ania vitendo vya uovu ikiwemo mauaji, ushirikina,uchoyo, ubinafsi na usengenyaji hivyo wanatakiwa watoke huko waje kwenye nuru.
Akizungumza hayo alipokuwa kwenye misa ya mkesha wa sikukuu ya Pasaka, Makubi alisema ufufuko wa bwana Yesu Kristu ni ushindi dhidi ya kila aina ya uovu watu wamkiri ili waweze kuuona ufalme wa mbinguni.
Makubi amesema walipoanza ibada walianza na giza hivyo katika giza kuna hatari kwani hakuna mtu atayehakikishia usalama wa mtu.
"Kanisa linatuambia msifanye yale ambayo yapo kinyume na Mungu tumeona bado watu tumeng'ang'ania na tabia zetu za ubaya kama ushirikina,uchoyo, mauaji na ubinafsi, kwa nini tunamng'ang'ania shetani utoke huko uliko uje kwenye nuru," amesema Makubi.
Padre Makubi amesema katika kitabu kitakatifu cha biblia, zaburi 17:5 inasema mtu asiyekuwa na matumaini huwa sawa na mtu aliyekuwa gizani.
No comments:
Post a Comment