Arusha. 

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dk Solomon Masangwa leo Jumatano, Machi 3, 2020 ameongoza ibada ya mazishi ya  mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Endrew Mollel ambaye alikuwa mwanzilishi  na mkurugenzi wa kampuni kadhaa mkoani Arusha .

Akizungumza katika ibada ya mazishi ya mfanyabiashara huyo, alisema Arusha na familia imempoteza mtu shujaa, hodari na mtu imara kama lilivyo jina lake.

Hata hivyo, alitaka familia ya Mollel kuenzi mambo mema aliyokuwa akifanya, kuimarisha umoja na mshikamano katika familia, ikiwepo kumtuza mjane ambaye ameachwa na mfanyabiashara huyo.

Alisema waumini wa kanisa la KKKT, mjini Kati wamepoteza muumini mzuri ambaye kila siku ya ibada alikuwa viti vya mbele na mkewe na alikosekana tu alipokuwa safarini.

Ibada ya kumuaga mfanyabiashara hiyo na mazishi pia yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwepo, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, Katibu Mkuu  msaafu wa CCM Abdrahman Kinana.

Mfanyabiashara huyo, amezikwa katika makaburi ya familia eneo la Olorieni katika jiji la Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya watu, wakiwepo wafanyakazi wa kampuni zake, ndugu, jamaa na marafiki.

 Mollel alikuwa ni mkurugenzi wa kampuni ya Happy Sausages  Ltd, Kijenge Animal Product Limited, Georges Center LTD and AGM Holding  pia mjumbe wa bodi mbalimbali hapa nchini.

Wakati huo huo, mkurugenzi wa kituo cha Radio ORS, Martin ole Sanago ambaye pia alikuwa mkurugenzi na mwanzilishi wa mashirika na taasisi mbalimbali anatarajiwa kuzikwa Ijumaa nyumbani kwake Terati wilayani Simanjiro.

Mdogo wa marehemu, Gidioni Sanago amesema taratibu za mazishi tayari zimeanza nyumbani kwake Terati ambapo ibada na salamu za rambirambi zitatolewa.

ASKOFU MASANGWAAONGOZA MAZISHI YA MFANYA BIASAHARA MAARUFU ARUSHA ASEMA NI SHUJA

No comments:

Post a Comment