Arusha
Mtangazaji wa Habari Maalum Media ambaye amekuwa akifanya Vipindi mbalimbali katika Kituo hicho Method Charles amefanikiwa kuwa Balozi mpya wa shirika lisilo la Kiserikali la Builders of Future Afrika (BFA) ambalo limekuwa likijihusisha na kuwasaidia Wanafunzi ambao hawana uwezo Wa kumudu Mahitaji Muhimu Mashuleni Katika Maeneo ya Mijini na Vijijini.
Akizungumza Mara Baada ya Kumtangaza kuwa balozi wa Shirika hilo Mkurugenzi wa wa Builders of Future Africa Elisante Ephraim amesema Method Charles amekuwa akifanya kazi mbalimbali za Kijamii hivyo wanaamini kupitia kazi zake anazo zifanya ataitangaza vema (BFA) kwa jamii juu ya Kazi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na Shirika hili.
Kwa Upande wake Method Charles Balozi Mpya wa BFA amesema kuwa Tanzania bado kuna kundi kubwa la Vijana ambao wana uwezo wa kufanya Vizuri katika Masomo lakini kwa sababu za Kimazingira Wanashindwa kufanya Vizuri kupitia kazi hiyo ya Ubalozi ambao ameupata ataitangaza BFA ili kupata watu watakao ungana kwa pamoja kusaidia kundi hili kufikia Malengo.
“Katika Jamii kuna makundi ambayoyanahitaji watu kufikia Malengo yao na Watu ndio sisi ni vema Zaidi Vijana wasomi kuamka na kusaidia Vijana wenzetu walio mashule katika shule ya Msingi, Sekondari na Hata Vyuoni Kuwasaidia kufikia Malengo yao kwa kutoa Hata kama kidogo ulicho nacho kwani hata Ulipo sasa Ulishikwa Mkono na Mtu” Alisema Method Charles Mtangazaji wa Habari Maalum Media.
Aidha Charles amewaomba Vijana ambao wamehitimu masomo yao na Kuajiriwa au Kujiajiri kulifikiria Kundi hili la Vijana ambao wana uwezo wa Kimasomo lakini hawana uwezo wa Kumudu mahitaji yao kimasomo kwa kujitoa kuwachangia hata kama ni Vifaa ya Shule, Ada, Mavazi ili kusaidia kufikia ndoto zao.
Amesema BFA ipo Tanzania nzima wamekuwa wakisaidia wanafunzi ambao hawana uwezo wa kumuda mahitaji Muhimu mashuleni na kwa wale watakao hitaji kuanza kuchangia wanaweza kuwasiliana na Mkurugenzi wa Shirika hilo Ndug Elisante Ephraim ili kuwashika Mkono Wanafunzi walio katika kundi hili Kufikia Malengo.
Method Charles ni Mwandishi wa Habari za Uchunguzi na Tija kwa jamii, Mwanzilishi wa Kampeni ya Karabati Shule yako aliyo ianzisha Mwaka 2018 ambayo ilizaa matunda kwa wananchi kujitoa katika Baadhi ya Shule wilayani Arumeru kwa Kukarabati Shule zao na pia ni Mtangazaji wakipindi cha asubuhi kinacho husiana na Masuala ya Kijamii Habari Maalum Fm 97.7.
CHANZO CHA HABARI
MKURUGEZI WA BFA
ELISANTE EPHARIM
CONTACT : +255764339147
No comments:
Post a Comment