Muhubiri wa Injili Barani Afrika na Mwazilishi wa kanaisa la Prophetic Latter Glory Ministry International ameoneka sana Wiki hili kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha akiwa amewasili nchini Nigeria kwa ajili ya kueneza neno la Mungu.
Alipokelewa vyema huku akiwa na ulinzi mkali kando yake jambo ambalo lilikusudia wanamitandao kuzua mjadala na gumzo mitandaoni.
Mnamo Alhamisi Natasha aliwaarifu mashabiki wake kuwa anasafiri na kuelekea nchini Nigeria.
Kupitia kwenye mitandao hiyo muhubiri huyo aliwafahamisha pia mashabiki wake kuwa amewasili vyema na amepokelewa vyema.
Baada ya picha hizo wanamitandao hawakulaza damu bali wali hoji huku wengi wakidai kuwa hatakiwa kuwa na walinzi kwa maana Mungu alisema kuwa atatulinda kila mahali tuendapo.
Natasha na wenzake walikuwa wamealikwa na askofu Samuel Blessing, Natasha alipendezwa na upokezi ambao askofu alikuwa ameuandaa huku akimshukuru kwa hayo yote.
No comments:
Post a Comment