Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuhimiza jamii kusimamia maadili katika maeneo yao ili kuendelea kudumisha amani ya nchi ili kuepuka vitendo visivyofaa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwinjilisti Dk. Dana Morey kutoka Marekani (USA) ambaye amewasili jijini Dodoma kwa ajili ya mkutano wa kimataifa wa mavuno na miujiza amewasihi wakazi wa Dodoma kutumia mkutano huo kama fursa ya kubadilisha mtindo wao wa maisha.

 Dr. Morey amempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kushirikiana na viongozi wa dini pamoja na watanzania kwa kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.

Hata hivyo kwa upande wake Mratibu wa mkutano Mchungaji Dk. Vangast Salum wa Kanisa la T.A.G (URCC) ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kujitokeza katika mkutano huo ambao utawajenga kiimani na kuwa na hofu ya MUNGU.

JAMII YATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KIDINI KATIKA MAENEO YAO

No comments:

Post a Comment