Raia wa Tunisia ambaye aliua watu watatu kanisani nchini Ufaransa, amekutwa na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19, jambo ambalo limechelewesha mahojiano, mtu aliye karibu na uchunguzi ameeleza.
Brahim Issaoui, 21, anaendelea kubakia hospitalini kutokana na kushambuliwa kwa risasi kadhaa na polisi baada ya kufanya shambulio kwa kutumia kisu katika kanis.
"Bado hajahojiwa, uchunguzi wake bado haujawekwa bayana," mtu mwingine aliye katika uchunguzi aliiambia AFP Jumatatu mchana.
Issaoui, ambaye anajulikana na polisi nchini Tunisia kwa vurugu na makosa yanayohusiana na dawa za kulevya, aliwasili Ufaransa mwezi uliopita, akiwa amevuka bahari ya Mediterranean kupitia kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.
Awali vyombo vya habari nchini Italia vilisema awali aliwekwa katika karantini pamoja na wahamiaji wengine wapatao 400 waliokuwa katika boti, kabla ya kuruhusiwa kushuka Bari Oktoba 9.
Wachunguzi wamebaini kuwa aliwasili Nice Oktoba 27, siku mbili tu kabla ya shambulio hilo kanisani.
Mwanamke mmoja alikatwa koromeo na mfanyakazi wa kanisani pia aliuawa kwa kuchomwa kisu ndani ya kanisa, wakati mwanamke mwingine alimudu kutoroka lakini akafariki baadaye kutokana na majeraha.
Polisi walisema Issaoui alipiga kelele akisema "Allahu Akbar" (Mungu mkubwa) wakati wakimkamata, kitu kilichofanya maofisa kusema tukio lake lilikuwa ni shambulio la waumini.
No comments:
Post a Comment