Na Method Charles

Uongozi wa kanisa katoliki umesema matamshi ya Papa wakati wa mahojiano kwenye filamu ya Francesco ambayo ilipeperushwa kwa mara ya kwanza Jumatano, Oktoba 21, yalihaririwa.
Kulingana na Daily Mail, matamshi ya kiongozi huyo yaliunganishwa pamoja na mahojiano yake ya awali na hivyo kuzua sintofahamu.
 
"Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, Papa Francis alijibu maswali mawili tofauti wakati tofauti, katika filamu hiyo, lakini yalihaririwa na kuchapishwa upya kama jibu la swali moja bila kuchunguza kwa makini na kupelekea sintofahamu," ilisoma taarifa kutoka Roma.
 
Vatican ilisema Francis alikuwa akikariri msimamo wake wa mwaka 2010 ambapo alipinga vikali ndoa ya wapenzi wa jinsia moja wakati huo akiwa askofu mkuu wa Buenos Aires.
 
Katika mahojiano ya awali, kiongozi huyo wa kanisa Katoliki alisema wapenzi wa jinsia moja ambao wanataka kuingia katika ndoa ni watoto wa Mungu wenye haki ya kuwa na familia.
 
"Watu wanaoshirika mapenzi ya jinsia moja wana haki ya kuwa na familia.Ni watoto wa Mungu na wana haki ya kuwa na familia. Tunachotakiwa kufanya ni kuunda ni sheria ya umoja wa kiraia. ili kuwalinda kisheria," alinukuliwa Papa Francis na CBS News.
 
Mnamo 2016, Papa Francis aliwataka Wakristu kuomba jamii ya muungano wa kutetea haki za mashoga na wasagaji (LGBT) msamaha kwa kuwatendea matendo ya kinyama kwa miaka na mikaka.
Papa huyo alishtumu kubaguliwa kwa wapenzi wa jinsia moja akisema wanatakiwa kuheshimiwa kulingana na mafundisho ya bibilia.
 
Mnamo 2013, alinukuliwa akisema hawezi kumhukumu yeyote kutoka jamii hiyo ambaye anamtafuta Mungu.
 
VATICAN YATOA UFAFANUZI KUHUSU PAPA FRANCIS KUUNGA MKONO USHOGA

No comments:

Post a Comment