Muimbaji wa
nyimbo za Injili, Bahati Bukuku ameridhia aliyekuwa mumewe Daniel Basila
kuoa mwanamke mwingine kwani walishapeana talaka siku nyingi.
Bahati ameongea hayo baada ya kupata habari kuwa mumewe amepata
mchumba anayeitwa Elizabeth Ngaiza na wanatarajia kufunga ndoa hivi
karibuni.
“Unajua kwanza ndio nazipata habari hizi za mume wangu kuoa lakini
sina kipingamizi kwani nilishaachana naye siku nyingi na alinipa talaka
rasmi mahakamani Julai mwaka huu, hivyo sioni tatizo kabisa,” alisema
Bahati.
Hata hivyo ndugu wa karibu na familia hiyo aliyeomba hifadhi ya jina
lake alisema kuwa, mume wa Bahati kwa sasa ameamua kuhama kabisa na
kwenda kuchumbia mkoani kwani yeye na Bukuku walikaa mbali kwa miaka 14
ambapo kwenye ndoa yao walipata mtoto mmoja ambaye alifariki.
“Daniel na Bahati walikaa kwenye ndoa kwa muda mfupi sana,
walitengana kwa miaka 14, kila mmoja akijua ipo siku watarudiana kwani
walikuwa na ndoa ya kanisani lakini baada ya Daniel kushindwa kuvumilia,
ameamua kumpa talaka mkewe na sasa ndio amechumbia ili aingie tena
kwenye ndoa,”
alisema ndugu huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Eliza na Daniel walikutana mkoani Dodoma ambapo walikuwa wameenda
kutoa huduma kwani Eliza naye ni muimba Injili kama alivyo Bahati
Bukuku.
“Wawili hao walivyokutana kwenye huduma walibadilishana namba za simu
ambapo Eliza hakujua kuwa ni mtaliki wa Bukuku, wakaanzisha uhusiano
uliozaa uchumba na sasa wanaelekea kwenye ndoa,” alisema ndugu huyo.
Stori: Neema Adria,
No comments:
Post a Comment