Na Method charles
Wataalamu
wa masuala ya nishati kutoka nchi za kusini kwa jangwa la Sahara
wamekutana jijini Arusha kujadili upatikanaji endelevu wa nishati
mbalimbali katika nchi hizo na kuangalia namna ya kufanya biashara kwa
nchi wanachama ili kutatua tatizo la uhaba wa nishati.
Meneja
miradi kutoka Tanesco Steven Manda ameyasema hayo katika mkutano huo
ambapo amesema lengo ni kuangalia jinsi ya kuhakikisha nishati endelevu
inapatikana katika nchi hizo.
Kwa
upande wake meneja udhibiti wa nishati nchini Switzerland Wilson
Masango amesema kuwa nchi za Afrika zinapaswa kufikiria juu ya kuuza
umeme ambao huzalishwa ili kuziba lengo kwa nchi zenye uhaba wa
nishati.
Naye
MKURUGENZI mtendaji wa kampuni ya Songas Nigel Whittaker amesema kuwa
kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na tanesco ili kuhakikishi
watanzania wanapata nishati kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment