Mchungaji Jeremia Mollel wa kanisa la TAG OLmuringaringa Mkoani Arusha nchini Tanzania amesema atawafukuza waumini ambao wataendeleza Mila na Desturi za Kimasai badala ya kumuamini Yesu pekee licha ya kuijua kweli.
Hayo ameyasemwa
katika ibada ya Jumapili wakati akizungumza na waumini
wake wa Kanisa hilo.
Mchungaji Jeremia
amesema kuwa kujiingiza katika katika mila na desturi ni
kuabudu Miungu Mingine na Kuvunja amri za Mungu.
Aidha ametaja
Mila hizo ni pamoja na Mwanamke kumnyoa Upala Mume wake anapokuwa ametimiza
Miaka saba ndani ya Ndoa .
Hata hivyo
ametaja Mila nyingine ya Kimasai ambayo ameipiga Marufuku ni kumuweka Mama
mzazi mwaka mmoja anapokuwa amejifungua huku akichinjiwa Mbuzi na Kondoo.
Kwa Mujibu wa
Kitabu cha Kutoka sura ya ishirini mstari wa tatu Biblia inasema usiwe na
Miungu Mingine ila mimi yaani Mungu.
No comments:
Post a Comment