Serikali imesema ipo katika mchakato wa
kutafuta muwekezaji mwingine katika awamu ya pili ya mradi wa mabasi ya
mwendokasi ikiwa kama njia ya kujaribu kutatua changamoto za usafiri
katika Jiji la Dar es salaam.
Hayo yamesemwa Bungeni leo Mei 10, 2018
na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa katika kipindi cha maswali na majibu
na kusema kuwa serikali ikiongeza muwekezaji mwingine katika mradi huo
itasaidia kuleta ushindani wa kibiashara baina ya makampuni hayo na
hatimaye wananchi watapata huduma bora ya usafiri.
"Tunaendelea kuondoa changamoto za
muendeshaji aliyopo sasa, lakini tumeanza utaratibu wa kupata
muendeshaji mwingine ili tupate kampuni nyingine iingize mabasi yake,
kuimarisha usafiri wa Jijini Dar es salaam lakini suala la miundombinu
tutaimalisha na tunajipanga vizuri ili kuhakikisha huduma hii inaendelea
kuwanufaisha watanzania", amesema Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa aliongezea kuwa serikali itachukua hatua kwa muwekezaji wa sasa kama akishindwa kuendesha mradi huo.
"Pale ambapo itabainika muendeshaji wa
sasa anamatatizo yaliyokithiri, hatuna shida tutamuondoa kwasababu
waendeshaji wapo wengi, wapo watanzania na mataifa ya nje wanaweza
kuendesha na kuleta mabasi", amesisitiza Majaliwa.
Kumekuwepo na changamoto mbalimbali
katika uendeshaji wa maradi huo ikiwemo mgogogro kati ya UDART na
kampuni ya ukatishaji tiketi ya za kielektroniki, ubovu wa miundombinu
katika ofisi za kampuni hiyo hasa kipindi cha mvua na changamoto ya
uchache wa mabasi kwa abiria wakati wa asubuhi na jioni.
Mradi wa mabasi ya mwendokasi kwasasa
unasimamiwa na serikali kupitia shirika la usafiri UDA kwa kushirikiana
na kampuni binafsi ya DART na kuunda kufanikiwa kuunda kampuni moja ya
UDART.
No comments:
Post a Comment