Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Roberto Firmino Barbosa de Oliveira
(Roberto Firmino), amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu
ya Liverpool ambayo ilimsajili mwaka 2015 akitikea 1899 Hoffenheim ya
Ujerumani kwa ada ya Pauni milioni 29.
Mshambuliaji huyo ambaye tayari ameshaifungia Liverpool mabao 27
katika michuano yote aliyocheza msimu huu, amefikia maamuzi ya kukubali
kusaini mkataba huo, baada ya kukamilisha mazungumzo na viongozi wa juu
huko Anfield.
Kabla ya kusaini mkataba mpya, mkataba wa awali wa Firmino mwenye
umri wa miaka 26, ulitarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu 2019-20.
No comments:
Post a Comment