Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekosolewa vikali na wadau wa
mitandao pale alipomtaka Waziri wa Fedha kutafuta njia ya kutoza kodi
mitandoa ya kijamii, ili kuzuia kile alichokiita ni “umbeya” unaoenezwa
na mitandao hiyo.
Maafisa wa serikali ya nchi hiyo wamesema kuwa wamejadiliana kwa kina
kuhusu kauli hiyo, hivyo wanafanya juhudi kuanza kutoza kodi kwa data
inayotumika kwenye simu kila siku kuanzia July 2018.
Aidha, Serikali ya Uganda imesema kuwa matumizi ya intaneti katika
simu yameongezeka kwa asilimia 15 mwaka uliopita wakati watu wengi zaidi
wamekuwa wakitumia huduma za mitandao kwa ajili ya huduma hiyo na
kufanya malipo.
“Nafikiri siku hizi, kwa hakika kuna idadi kubwa ya wafanyabiashara
ambao wanatumia tu mtandao wa Instagram na Whats App na njia mbali mbali
ambazo wanajitangaza kupitia intaneti, Kwa hiyo nafikiri tathmini ya
rais ilikuwa haitendei haki malengo ya wale wanaotumia mitandao
hiyo,”amesema Blogger Godiva Akullo.
Hata hivyo, Maafisa wa Baraza la Mawaziri wanatetea mapendekezo hayo
ya kodi, kwamba itasaidia kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya simu.
No comments:
Post a Comment