Mwalimu wa Sekondari ya Nyambureti wilayani Serengeti, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumtorosha mwanafunzi wa kidato cha pili kwa zaidi ya siku nne.
Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Juma Shija alikiri kushikiliwa kwa mwalimu huyo na kwamba alikamatwa Mei 2.
Hata hivyo, mwalimu huyo amekana kuwa na
uhusiano na mwanafunzi huyo na kwamba hizo ni hila za baadhi ya watu
kutaka kumharibia kazi.
Naye mkuu wa wilaya hiyo, Nurdin Babu
alisema mtuhumiwa anadaiwa kumtorosha mwanafunzi huyo wakati wanatoka
kwenye michezo ya Umiseta na kukaa naye kwa siku nne.
“Mwalimu hakuonekana kazini kwa siku nne
na mwanafunzi halikadhalika, wazazi wakaanza kumtafuta na baada ya
kuonekana na kubanwa mtoto alieleza alikuwa kwa mwalimu kwa kuwa ni
mpenzi wake,” alisema Babu.
Babu alisema baada ya mtoto kutoboa siri
wazazi walikusanyika wakitaka kumshambulia mwalimu huyo hali
iliyoufanya uongozi wa wilaya kutuma polisi ili kumnusuru na kumkamata
ili aweze kueleza kwa undani.
“Mtoto huyo anadai kuwa walianza
uhusiano Oktoba 25, 2017 akiwa kidato cha kwanza na kuwa mke wake
akienda masomoni yeye anaendelea naye, kitendo hiki hatuwezi kukivumilia
lazima afikishwe mahakamani,” alisema.
Alisema wanaume wakware hawatavumiliwa kwa kuwa wanawaharibia watoto maisha yao.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwa mwaka jana zilikuwapo mimba zaidi ya 25 kwa shule za msingi na sekondari.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,
Juma Hamsini amemsimamisha kazi mwalimu huyo kutokana na tuhuma hizo za
utovu wa nidhamu na kuitaka polisi kuhakikisha inamfikisha mahakmani.
No comments:
Post a Comment