Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa,
Charles Kabeho amegoma kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi
wa halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kwa madai kuwa thamani ya fedha
za ujenzi zilizotumika haziendani na nyumba hizo.
Tukio hilo limetokea leo Mei 8,2018
baada ya kiongozi huyo kutembelea mradi huo wakati mwenge wa Uhuru
ukikimbizwa wilayani Kalambo huko mkoani Rukwa.
Hata hivyo kiongozi huyo ameitaka
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mradi huo
unaotajwa kuwa na thamani ya Sh511milioni,akibainisha kuwa kuna
matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi huo
uliyotolewa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kalambo, Simon
Kagani amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa Julai 2016 na
kukamilika Aprili 2017 na kugharimu kiasi hicho cha fedha, ambapo
Serikali Kuu imechangia Sh496milioni, halmashauri Sh15milioni.
Akitaja sababu za kutozindua mradi huo
ni kwa kuwa amebaini thamani ya fedha haifanani na nyumba zilizojengwa
na kwamba milioni 500 imetumika kujenga nyumba tani ambazo hazina
thamani hiyo.
No comments:
Post a Comment