Katibu
Mkuu wa chama cha Wafanyakazi nchini (TUCTA), Yahaya Msigwa
amezungumzia kauli ya Rais Magufuli juu ya kutoongeza mshahara kwa
wafanyakazi, jambo ambalo limeonekana kuibua hisia hasi kwa watu wengi
wakiwemo wanasiasa na wafanyakazi.
Msigwa
amesema kuwa wao kama wawakilishi wa wafanyakazi, wanakusudia kufanya
kikao maalum kujadili suala hilo, na kisha kulijadili na serikali
kuangalia njia mbadala na muafaka.
“Mambo
ya mishahara ni mambo ya utatu yaani wafanyakazi, waajiri na serikali,
na mambo haya yanahitaji kujadili kwenye bodi, wafanyakazi wangependa
kila mwaka kama inawezekana wawe wanapandishiwa mshahara, kwa hiyo hilo
tutalijadili kama wafanyakazi halafu badaye tutajadiliana nao serikali”,
amesema Msigwa.
No comments:
Post a Comment